Monday, April 29, 2013

HISTORIA YA UKWELI KUHUSU PALESTINA

Ulimwengu wetu wa sasa umekuwa ni wa utandawazi (ulimwengushi) kwa kiasi ambacho yaliyo ndiyo yamekuwa siyo na ya makosa yamechukuliwa kuwa ni ya makosa. Ulimwengu umekuwa ukipigwa makombora na vyombo vya habari kwa njia moja au nyingine.
 
Mwenye kumiliki chombo cha habari cha kilimwengu anaweza kupeperusha au kuandika ya kwake na yakaweza kuchukuliwa kama ukweli mtupu. Ulimwengu umekuwa ni wenye kuchukua yote na wenye sauti kubwa kwa kuwa na vyombo hivyo wameweza kusikika mbali  japokuwa hawana haki wa kupata wanayopata.
 
Kadhiya moja ambayo imeeleweka sivyo ni kadhiya ya historia ya Palestina. Waliojizatiti kuiweka katika hali hiyo iwe hivyo ni WAZEYUNI bila kuwa na pingamizi kwa kuwa na sauti kubwa. Juhudi dhidi yao zimekuwa zikifanywa bila ufanisi wowote kwa sababu ya sauti kubwa waliyonayo wao. Taasisi kubwa na maarufu za vyombo vya habari zinamilikiwa nao kwa namna moja au nyingine. Mbali na hiyo hatufai kufa moyo kuhusu juhudi hizo kwani nusura hutokea baada tawfiki ya Allaah Aliyetukuka, kisha juhudi zetu kwa kutumia njia tofauti.

FACEBOOK AU FITNABOOK


Kwanza kabisa, ijulikane wazi kwamba kusudio la makala hii si kutoa fatwa wala hukumu. Lengo ni kuweka wazi manufaa na madhara ya Facebook ili mtu binafsi atoe hukumu yake mwenyewe.
Je, ni Facebook au Fitnabook? Hili ni suali ambalo watu wengi wameanza kujiuliza baada ya kujionea  vitimbi na kashfa kadhaa katika huu mtandao ambao unazidi kujipatia umaarufu kila pembe ya dunia. Naam, kuna vitimbi kadhaa vinafanyika kwa jina la Facebook. Na ndio kuna vijana wengi ambao wametumbikia katika janga la fitna katika Facebook lakini nini suluhisho la hili? Kabla hatujatazama hebu kwanza tuangalie manufaa na madhara ya Facebook.

Manufaa
Kama ilivyo kawaida ya vitu vingi, Facebook ina faida yake. Lakini je, hizo faida ni nyingi kuliko madhara? Katika sehemu hii tutaja manufaa ambayo yako wazi kutokana na utumiaji wa Facebook. Manufaa hayo ni kama yafuatayo:
1.     Kufanya da’wah ( kuwalingania watu kwenye Uislam)
Madaa’iyah kadhaa pamoja na baadhi ya Mashaykh hutumia Facebook kwa kazi za da’wah. Huwekwa na kutumwa vitu mbalimbali vya kufikisha mafunzo mbalimbali ya Dini kama: video za mawaidha, makala za Kislamu na njia mbalimbali za kunufaisha wasomaji. Endelea.........


ALJAZEERA YAFUNGIWA IRAQ

Seriakli ya Iraq imekifungia kituo cha televisheni cha kimataifa cha Aljazeera na vituo vingine tisa vya nchini humo siku ya Jumapili, baada ya kivituhumu kwa kuchochea vurugu za kidini.
Hatua hii imemulika wasiwasi unaozidi wa serikali inayoongozwa na washia, juu ya hali ya usalama inayozidi kudorora, wakati wa machafuko ya waumini wa kisunni na makabiliano yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 180 katika muda wa chini ya wiki moja. Kusimamishwa kwa vituo hivyo ambako utekelezaji wake ulianza mara moja kunaonekana kuvilenga hasa vituo vya kisunii vinavyojulikana kwa kuikosoa serikali ya waziri mkuu Nouri al-Malik. Pamoja na kituo cha Aljazeera, uamuzi huo uliviathiri vituo nane vya kisunni na kimoja cha kishia. hatua hii ya serikali imekuja huku utawala mjini Baghdad ukijaribu kukabiliana na ongezeko la machafuko nchini humo, yaliyoripuka siku chache zilizopita, baada ya vikosi vya usalama kuanzisha operesheni ya ukandamizaji dhidi ya kambi ya waandamanaji wa kisunni katika mji wa kati wa Hawija, na kuua watu 23, wakiwemo wanajeshi watatu.
Tangu wakati huo, zaidi ya watu 180 wameuawa katika mapigano na vikosi vya usalama na mashambulizi mengine. Wimbi la hivi karibuni la vurugu linafuatia miezi minne ya maandamano ya amani ya waislamu wa madhehebu ya sunni, dhidi ya serikali ya waziri mkuu Nouri al-Maliki. Watazamaji nchini Iraq watanedelea kutizama vituo hiyvo, lakini tangazo la kusitishwa kwake lililotolewa na tume ya mawasiliano na vyombo vya habari linasema kama vituo hivyo kumi vitajaribu kuendesha shughuli zake katika ardhi ya Iraq, vitakabiliwa na hatua za kisheria kutoka kwa vyombo vya usalama. Kimsingi amri hiyo inawazuia wanahabari kutoka vituo hivyo kufanya kazi zao nchini Iraq.

ITALIA KUPUNGUZA MISHAHARA YA MAWAZIRI

Waziri mkuu mpya wa Italia, Enrico Letta, amesema kuwa hatua ya kwanza kufanywa na serikali yake itakuwa ni kuondoa mishahara ya mawaziri ambao pia ni wabunge ambao kwa sasa wanapokea mishahara miwili. Akilihutubia bunge la Italia, Letta amesema katika kuonyesha mfano, serikali lazima ifute mishahara kwa mawaziri ambao pia ni wabunge. Hatua hiyo ni katika kujibu hasira ya wananchi wa Italia kuhusu wanasiasa wenye mishahara miwili wakati ambapo nchi hiyo inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi.

UGIRIKI YAPUNGUZA AJIRA 15,000

Bunge la Ugiriki limepitisha hatua zaidi ya kubana matumizi, ikiwemo kupunguza nafasi 15,000 za ajira ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao wa 2014. Sheria hiyo pia imerefusha kodi ya mali kwa mwaka mmoja mwingine. Baada ya mjadala wa siku moja, serikali ya Ugiriki imepitisha sheria yenye kurasa 110 katika kifungu kimoja. Wakopeshaji wa kimataifa wa Ugiriki wanaitaka nchi hiyo ipunguze gharama zake kabla haijapatiwa msaada wa Euro bilioni 8.8 kwa ajili ya kuuokoa uchumi wake. Hata hivyo, wananchi wa Ugiriki wameingia mitaani kwenye mji mkuu wa Athens, kupinga hatua hiyo ya serikali ambayo ni ndogo kuliko ilivyotarajiwa.

VIINI SUGU VYA MALARIA VYAGUNDULIKA

Aina mpya ya viini sugu vinavyosababisha Malaria na ambavyo havisikii dawa vimegunduliwa na wanasayansi. Watafiti wamevigundua viini hivyo Magharibi mwa Cambodia na wanasema kuwa vina umbo tofauti la genetiki ikilinganishwa na viini vingine duniani.   Viini hivi ni sugu kiasi cha kutosikia dawa aina ya Artemisinin, dawa yenye nguvu zaidi katika kutibu Malaria.
Taarifa ya kwanza kuwa wagonjwa walikuwa hawatibiki na dawa hiyo ilitokea mwaka 2008. Tatizo hilo tangu hapo limeenea katika maeneo mengine ya Asia ya Kusini. Utafiti huu umechapishwa katika jarida la ''Nature Genetics.'' Mtafiti mkuu Daktari Olivo Miotto, wa chuo kikuu cha Oxford na kile cha Mahidol nchini Thailand,amesema kuwa dawa zote zenye uwezo wa kuua Malaria na ambazo zimevumbuliwa katika miaka ya hivi karibuni, zimekuwa ovyo katika kutibu Malaria.
"Dawa ya Artemisinin kwa sasa inafanya kazi vyema. Ndio silaha nzuri zaidi dhidi ya ugonjwa huo na tunahitaji kuendelea kuitumia,'' alisema Daktari Miotto. Magharibi mwa Cambodia kumetajwa kama sehemu yenye Malaria sugu. Haileweki ni kwa nini tangu mapema miaka ya 1950, viini vya Malaria katika eneo hilo, vimekuwa sugu. Tatizo hilo pia limesambaa hadi katika sehemu kadhaa za Asia na Afrika.
Kwa sasa wanasayansi wana wasiwasi kuwa hali sawa na hiyo itajitokeza kwa dawa ya Artemisinin. Dawa hiyo inatumika kote duniani kukabiliana na Malaria, na inaweza kutibu ugonjwa kwa siku chache tu ikiwa itatumika na mchanganyiko wa dawa zengine.

SAYYED HASHEM: TUKO TAYARI KWA NJAMA ZA WAZAYUNI

Mkuu wa Baraza la Utendaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon Sayyed Hashem Safieddine amesema kuwa, Hizbullah imejiandaa kikamilifu dhidi ya njama na mipango ya uharibifu ya Marekani, Magharibi na Wazayuni. Sayyed Hashem Safieddine amesisitiza kuwa, kile kinachofanywa na Marekani huko nchini Syria si kingine ghairi ya uharibifu na kujaribu kuigawa nchi hiyo na kwamba, njama hizo hazitaishia katika mipaka ya Syria bali zitaenea katika nchi mbalimbali za eneo zikiwemo Iraq, Misri, Lebanon na Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Ameongeza kuwa, hivi sasa njama kubwa zinazofanywa na Marekani na Magharibi ni kuwasha moto wa mapigano ambao utaziteketeza nchi za eneo na kwamba, kama ilivyo ada Harakati ya Mapambano ya Hizbullah haitaacha kukabiliana na njama hizo kwa kutumia silaha yake iliyo huru na ambayo ilipata nguvu baada ya vita vya siku 33 na adui Mzayuni. Aidha ameashiria vitisho vya Wazayuni dhidi ya Lebanon vinavyotokana na madai ya kutungua ndege isiyo na rubani inayodaiwa kumilikiwa na harakati ya Hizbullah ya Lebanon karibu na bandari ya kaskazini mwa Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, na kuongeza kuwa, Israel inafahamu vizuri kuwa, vitisho vyake hivyo havina taathira yoyote kwani muqawama umejiandaa vilivyo kujibu hujuma yoyote ile.

WAZIRI MKUU WA SYRIA AKOSWA NA BOMU

Habari kutoka Damascus nchini Syria zinasema kuwa msafara wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Wael al-Halki umeshambuliwa mapema leo lakini kiongozi huyo hakujeruhiwa. Habari zaidi zinasema kuwa shambulio hilo la bomu limesababisha kifo cha mlinzi mmoja wa Waziri Mkuu huyo. Kanali ya al-Akhbariyah imeonyesha video baada ya shambulio hilo katika eneo la Mezze ambapo majumba kadhaa yamevunjika madirisha kutokana na uzito wa milipuko hiyo. Rais Bashar Asad amelaani shambulio hilo na kuapa kuendeleza mapambana dhidi ya magaidi wanaojaribu kuvuruga nchi kwa msaada wa Wamagharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu. Wael al-Halki baadaye ameonekana akiongoza mkutano wa wanauchumi ofisini kwake akiwa mzima wa afya

GENGE LA MAGAIDI LAKAMATWA IRAQ

Maafisa usalama wa Iraq wamekamata genge la magaidi baada ya kushindwa katika jaribio la kumuua afisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika wilaya ya al Adl mjini Baghdad. Magaidi hao walitaka kumuua afisa huyo kwa kutumia silaha zisizotoa sauti. Tukio hilo limejiri baada ya Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki kutahadharisha juu ya njama za kutaka kuirudisha nchi hiyo kwenye vita vya ndani. Mikoa kadhaa nchini huko inashuhudia makabiliano kati ya vikosi vya usalama na wanajeshi na wafuasi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaida na chama cha Baath.
Katika upande mwingine maafisa wa usalama wa Iraq wametangaza kuwa, watu karibu 20 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika milipuko mitatu ya kutegwa kwenye magari. Milipuko miwili kati ya hiyo imetokea kwa kufuatana katika mji wa Amara ulioko kilometa 200 kusini mashariki mwa mji mkuu Baghadad na mlipuko wa tatu umetokea kwenye mji wa Diwaniya kusini mwa Baghdad

HIZBULLAH WAPOKEA SILAHA HATARI TOKA SYRIA

Waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel, Binyamin Ben-Eliezer, amedai kuwa silaha za kemikali za Syria zinamiminika kwa kundi la wapiganaji la Hezbollah. Kauli hiyo ni ya kwanza kutolewa na mwanasiasa wa ngazi ya juu wa Israel. Ben-Eliezer, ambaye pia ameitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria na kumaliza mauaji ya raia, hakueleza ni wapi amepata ushahidi huo. Amesema mchakato wa kusafirisha silaha kwenda kwa Hezbollah, umeanza, ingawa amekataa kutoa ufafanuzi zaidi. Israel imerudia kuelezea wasiwasi wake kwamba silaha za kemikali za Syria, huenda zikaangukia mikononi mwa wapiganaji wanaoipinga Israel kama vile kundi la Hezbollah la Lebanon au kundi lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda, linalopigana na waasi wanaopambana na serikali ya Rais Bashar al-Assad.

Sunday, April 28, 2013

CHANGAMKIA NAFASI ZA MASOMO YA BURE NCHINI SAUDI ARABIA


Chuo cha King Abdulaziz kilichopo Jiddah nchini Saudi Arabia kinapokea maombi kutoka kwa wanafunzi kote duniani kwa ajili ya masomo ya kiarabu kwa miaka miwili (2 year Arabic scholarship program). Masomo yanatarajiwa kuanza mwezi wa tisa 2013 inshallah. Program hii inajumuisha huduma muhimu zifuatazo, malazi ni bure, milo mitatu kwa siku na pia chuo kitampatia kila mwanafunzi  pesa ya kujikimu ya mwezi mzima. Moja ya masharti muhimu ili uweze kukubaliwa kusoma katika chuo hicho na kupatiwa huduma kama zilivyoorodheshwa hapo juu, muombaji ni lazima awe ni MWANAUME na awe na umri kati ya miaka 17 hadi 25 TU. Kama huna vigezo hivyo hutapata kudahiliwa. Njia za kupata udahili ni kama zifuatazo:
1. Jaza fomu ya chuo kupitia mtandao kwa link ifuatayo,
2. Tuma barua pepe ya nyaraka zako muhimu kwa ali@kau.edu.sa  kupata taarifa ya nyaraka zinazohitajika, tazama link ifuatayo:
3. Kumbuka mwisho wa maombi ni alhamisi tarehe 15th MAY 2013.

GAZETI LA ANNUUR APRIL 26, 2013

BOUTEFLIKA AUGUZWA NG'AMBO

Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amesafirishwa na kupelekwa hospitali ya Paris baada ya kupata ugonjwa wa kiarusi kidogo. Wakuu wa Algeria wanasema Bwana Bouteflika alipelekwa Paris kufuata pendekezo la daktari wake lakini hali yake si ya kutia wasiwasi. Rais Bouteflika, mwenye umri wa miaka 76, anaonekana hadharani mara chache tu, na amekuwa akiuguwa kwa miaka kadha. Taarifa rasmi zinaeleza kuwa Jumamosi alipata ugonjwa wa kiarusi kidogo lakini haifikiriwa afya yake itaathirika kwa muda mrefu. Waziri Mkuu wa Algeria alisema hali ya rais siyo mbaya. Lakini kwa vile amesafirishwa na kupelekwa Paris, Ufaransa, watu wanauliza kama taarifa rasmi inaeleza ukweli.
Bwana Bouteflika alifanyiwa upasuaji kwenye hospitali mjini Paris miaka kadha iliyopita. Taarifa rasmi ilieleza kwamba alikuwa na kidonda cha tumbo; lakini nyaraka za siri za wana-diplomasi wa Marekani zilipofichuka zilisema kumbe alikuwa na saratani. Kuna watu wanaoamini kuwa Bwana Bouteflika anaweza kugombea muhula wane katika uchaguzi wa mwaka ujao, juu ya umri na afya yake. Yeye ni mmoja kati ya viongozi wakongwe ambao wameshikilia madaraka katika siasa za Algeria tangu nchi hiyo kupata uhuru kutoka kwa Ufaransa zaidi ya miaka 50 iliyopita.

WAPALESTINA WATAHADHARISHA NJAMA ZA WAISRAEL JUU YA ARDHI MPYA KWA WAPALESTINA

Walid al A’awadh Mjumbe wa Kamati ya Kisiasa ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) ametahadharisha juu ya njama za Wazayuni za kutayarishwa sehemu ya jangwa la Sinai la Misri kwa ajili ya makazi ya Wapalestina na kutangaza kuwa, eneo hilo kamwe halitokuwa nchi mbadala ya Wapalestina. Al A’awadhi amesema, watakabiliana vikali na kila mpango wa kuifanya nchi nyingine isiyokuwa ardhi yao asili ya Palestina kuwa nchi mbadala. Mjumbe huyo wa Kamati ya Kisiasa ya PLO ameongeza kuwa, kwa kisingizio cha kuwaounga mkono Wapalestina, wageni wanakusudia kuitenga sehemu ya Peninsula ya Sinai kama nchi yao mbadala, suala litakalozusha hitilafu nyingine kubwa kwenye eneo hilo.  Sambamba na kusisitiza kuunga mkono ardhi yote ya Misri afisa huyo amesema, katika kipindi chote cha historia Wapalestina daima wamesimama kidete kukabiliana na njama za maadui, na kwamba hawatofumbia macho haki zao halali kisheria. Kitambo nyuma pia kulizungumziwa mpango wa kuundwa nchi ya Palestina huko Misri, suala lililokabiliwa na radiamali kali ya Wapalestina. Wakati huo Mussa Abu Marzuq miongoni mwa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Wananchi wa Palestina (Hamas) ametangaza kupinga vikali Wapalestina mpango huo wa kuwahamishia katika jangwa la Sinai uliozungumziwa na duru za habari za Israel. Al Marzuq alipinga wazo la kuhamishiwa Wapalestina kwenye jangwa la Sinai na kusema kuwa, Wapalestina wanashikamana na ardhi zao na kwamba hawakubali eneo lolote badala yake. Sisitizo la Israel na waitifaki wake la kutekeleza mpango huo hatari wa kuwatafutia Wapalestina nchi mbadala linapignwa vikali na Wapalestina wenyewe na fikra za waliowengi duniani. Kuzungumziwa tena mpango wa nchi mbadala kwa ajili ya Wapalestina, kunadhihirisha kushtadi hatua za utawala huo na waitifaki wake za kuzuia kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Baitul Muqaddas. Israel kwa njia tofauti inakusudia kupora kikamilifu haki za Wapalestina na katika kutimiza hilo inataka kuwakosesha wananchi wa Palestina hata haki ya kuishi kwenye nchi yao. Kwa msingi huo, inatumia kila njia kuzuia uwezekano wa kuundwa nchi ya Palestina katika ardhi ya Palestina. Israel inataka kufanikisha hilo kwa kujenga kwa wingi vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kutenganisha maeneo ya Palestina na maeneo mengineyo kwa uzio wa kibaguzi. Pia sambamba na kuzungumzia suala hilo, utawala huo ghasibu unakusudia kuandaa mazingira ya kuwafukuza kabisa Wapalestina nchini kwao na kujaribu kupotosha kadhia ya kurejea wakimbizi wa Kipalestina kwenye nchi yao ili iweze kudhibiti kwa ukamilifu ardhi yote ya Palestina. Vilevile Israel inafuatilia mpango huo hatari wa nchi mbadala kwa ajili ya Wapalestina ili kufanikisha malengo yake ya kupenda kujitanua katika nchi za Kiarabu kama vile Misri. Kwa kuzusha wasiwasi miongoni mwa mataifa ya eneo la Mashariki ya Kati, utawala wa Kizayuni unataka kufaidika na hali hiyo na kupotosha fikra za waliowengi juu ya kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina. Kwa ujumla utawala wa Kizayuni kwa njia tofauti unataka kuwazuia Wapalestina na jamii ya kimataifa kufuatilia suala la kutekelezwa maazimio ya Umoja wa Mataifa, na pia Wapalestina kupata haki zao kisheria kukiwemo kuundwa nchi huru ya Palestina. Inasemekana kuwa, mengi kati ya maazimio yaliyopitishwa katika Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa Palestina yanasisitiza kuondoka Israel kwenye ardhi za Palestina na Wapalestina kupewa haki yao ya kuunda nchi huru mji mkuu wao ukiwa Baitul Muqaddas.     

WAASI NA SERIKALI YA SUDAN WASHINDWA KUAFIKIANA


Duru ya kwanza ya mazungumzo ya moja kwa moja ya amani baina ya serikali ya Sudan na waasi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan tawi la kaskazini imemalizika bila ya kuwa na natija. Taarifa zaidi zinasema kuwa, duru ya kwanza ya mazungumzo ya amani ya moja kwa moja baina ya serikali ya Khartoum na Harakati ya Ukombozi wa Sudan tawi la kaskazini ilifanyika jana kwa usimamizi wa Thabo Mbeki mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa na kumalizika bila natija yoyote. Kila upande miongoni mwa pande mbili hizo umeutuhumu upande wa pili kuwa ndio chanzo cha kushindwa mazungumzo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika mazungumzo hayo, Thabo Mbeki mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mazungumzo ya amani ya Sudan amesema kwamba, Khartoum na Harakati ya Ukombozi wa Sudan tawi la kaskazini wameshindwa kufikia mwafaka kuhusiana na ratiba ya mazungumzo yajayo.

ISRAEL YAJIBU MAPIGO TOKA GHAZA

Israel imejibu mapigo kwa makombora yaliyovurumishwa kutoka Ukanda wa Gaza kwa kufanya mashambulizi ya kutokea angani katika maeneo yanayotumiwa na wanamgambo wa kundi la itikadi kali za Kiislamu la Hamas, ambalo linadhibiti Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel limesema ndege zake zimelipua kituo kimoja cha kuhifadhi silaha za kundi la kigaidi na kituo cha kufanyia mazoezi cha Hamas. Hatua hiyo inakuja baada ya marokeoti kuvurumishwa kusini mwa Israel siku moja kabla. Pia jeshi hilo limefunga eneo moja muhimu la kuvuka mpaka, wakati maafisa wa afya katika Ukanda wa Gaza wakisema hakuna aliyejeruhiwa katika mashambulizi hayo.

ALQAEDA WATUHUMIWA KUWAUWA WANAJESHO WA YEMEN


Kundi la kigaidi la Al-Qaeda linatuhumiwa kuwaua wanajeshi watano wa jeshi la Yemen katika shambulio lililotokea huko kusini magharibi mwa mji wa sanaa. 
Mapema ijumaa wizara ya mambo ya ndani nchini Yemen ilisema imechukua hatua za tahadhari kufuatia taarifa za kiintelijensia za kuwepo kwa mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la al qaeda hatua ambayo haikuzuia mashambulizi hayo yaliyolenga kituo cha jeshi wilaya ya Rada. Maafisa wa serikali wamethibitisha kuuawa kwa wanajeshi watano na wengine kujeruhiwa. Katika mtandao wa wizara ya ulinzi nchini humo taarifa zimebainisha kuuawa kwa wapiganaji wawili wa al qaeda.

MAREKANI YATOA ONYO JIPYA KWA SYRIA


Rais wa Marekani Barack Obama ametoa onyo jipya kwa serikali ya Syria na kusema kuwa matumizi ya silaha za kemikali ni sawa na kubadilisha mchezo wakati huu ambapo Marekani inakabiliwa na shinikizo kubwa katika ardhi yake na mataifa ya nje kuhusu kuingilia kati mzozo huo wa Syria.
Siku moja baada ya maafisa wa Marekani kusema kuwa wanahisi kuwa silaha hizo za kemikali tayari zimekwisha kutumika katika mashambulizi madogo madogo, rais Obama ameonya kuwa Washington lazima ichukue hatua za busara, nakubainisha ukweli wa namna gani na kwa wakati gani silaha hizo zilitumika.
Obama, ambaye awali alimwambia rais wa Syria Bashar al Assad kuwa matumizi ya silaha za kemikali yatachora mstari wa hatari na kuahidi Marekani na jumuiya ya kimataifa kufanya uchunguzi wa kisayansi katika ripoti hii ya hivi karibuni.

Saturday, April 27, 2013

MSAMAHA KWA WAASI WA SUDAN

Makundi kadhaa ya waasi yanayoendesha harakati zao katika maeneo yenye utajiri wa mafuta kaskazini ya Sudan Kusini yamekubali pendekezo la msmaha wa serikali ili nao wasitishe uasi. Makundi ya waasi ya South Sudan Liberation Army, South Sudan Democratic Army na South Sudan Defense Forces, yote yamelikubali pendekezo hilo la msamaha la Rais Salva Kiir. Gazeti la Tribune limesema leo kuwa kundi la South Sudan Democratic Liberation Army, likiongozwa na David Yau Yau, ni kundi pekee lililougomea msamaha huo. Yau Yau anaongoza wapiganaji wa kabila la Murle, ambao wamekuwa wakipigana na serikali katika jimbo la Jonglei ambalo limekumbwa na mapigano makali ya kikabila katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Kwa ujumla, serikali ilitangaza msamaha kwa makamanda sita wakuu wa waasi na manaibu wao kwa kufanya uasi Makundi yaliyokubali msamaha huo yatakutana karibuni na Rais Kiir mjini Juba ili kukamilisha mpango huo na kuafikiana namna ya kuwajumuisha wapiganaji wao katika jeshi la kitaifa.

EU YAIKOSOA ISRAEL KUBOMOA NYUMBA ZA WAPALESTINA


Umoja wa Ulaya umeikosoa Israel kwa kubomoa majengo kadhaa ya raia wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ikiwemo al Quds ya Mashariki na hivyo kuwafanya mamia ya Wapalestina kubaki bila ya makazi. Umoja wa Ulaya umesema umesikitishwa sana na hatua ya utawala wa Tel Aviv ya kubomoa majengo 22 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan tarehe 23 na 24 za mwezi huu, hatua ambayo imepelekea raia wa Palestina 28 kubaki bila ya makazi miongoni mwao wakiwemo watoto 18. Ubomoaji huo wa utawala wa Kizayuni umewaathiri pia Wapalestina wengine 120 wakiwemo watoto 57. Ujumbe wa Umoja wa Ulaya uliotembelea Baitul Muqaddas na Ramallah umesema kuwa baadhi ya majengo yaliyobomolewa na Israel yalijengwa kwa ufadhili wa nchi wanachama wa umoja huo.
Nyumba na majengo mbalimbali ya Wapalestina zaidi ya 2,400 yamebomolewa katika eneo C huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Baitul Muqaddas ya Mashariki tangu mwaka 2008 na hivyo kusababisha raia wa Kipalestina zaidi ya 4,400 kuwa wakimbizi.

MUFTI : VILEVI VYOTE MARUFUKU


Mufti wa Libya ameitaka serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku vinywaji vyote vyenye kileo na madawa ya kuvya. Sadiq Al-Ghiryani amewataka viongozi wa serikali ya Tripoli kukabiliana na uuzaji wa vileo hadharani na madawa ya kulevya nchi humo. Al-Ghiryani amesisitiza juu ya ulazima wa serikali na viongozi wa Libya kupambana na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu na kuwataka Walibya wote wapambane na vitendo vilivyokinyume na mafundisho ya dini Tukufu ya Kiislamu, ukiwemo unywaji pombe na madawa ya kulevya.
Vilevile Mufti wa Libya amesema katika kuungana na familia dhidi ya vitendo viovu, serikali lazima ifunge mitandao yote ya internet ambayo inakinzana na maadili mema.
Kwa mujibu wa sheria za Libya, ni marufuku kutumia vinywaji vyenye kileo na dawa za kulevya na adhabu kali inatolewa kwa makosa hayo. Hata hivyo vileo na dawa za kulevya zimeongezeka kwa kiwango kikubwa nchini Libya kutokana na ukosefu wa usalama.

HALI YA HATARI KATI YA ISRAEL NA LEBANON


Jeshi la Lebanon limejiweka tayari kuanzia asubuhi ya leo kufuatia madai yaliyotolewa na utawala haramu wa Israel ya kudungua ndege isiyo na rubani katika anga ya mji wa Haifa inayodaiwa kumilikiwa na harakati ya Hizbullah.
Chanzo kimoja cha usalama katika jeshi la Lebanon kimesema kuwa, majeshi ya Lebanon yaliyoko katika mipaka ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo bandia yamewekwa katika hali ya tahadhari kubwa. Chanzo hicho pia kimesisitiza kuwa, jeshi la Israel limeongeza idadi ya askari wake hususan katika maeneo ya mashariki ya Mazariu Shaba'a na karibu na lango la Fatwimah huko Kufru Kalaa na eneo la Ghajar na kando na eneo la Abbasiyyah nchini Lebanon. Jeshi la utawala wa Kizayuni pia limeweka vifaru vya kivita aina ya Merkava katika maeneo kadhaa ya mpakani sambamba na kurusha idadi kadhaa ya ndege zake zizizo na rubani katika maeneo hayo.
Hapo jana jeshi la utawala haramu wa Israel lilitangaza kuwa, lilitungua ndege isiyo na rubani inayodaiwa kumilikiwa na harakati ya Hizbullah ya Lebanon karibu na bandari ya kaskazini mwa Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Hizbullah ya Lebanon imekanusha madai kuwa ilituma ndege isiyokuwa na rubani (drone) katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina huko Israel.

Friday, April 26, 2013

KOREA KUSINI YAONDOA WAFANYAKAZI WAKE KAESONG

Korea ya Kusini imesema itawaondoa wafanyakazi wake wote kutoka eneo la viwanda inalolimiliki pamoja na Korea ya Kaskazini. Uamuzi huo umefikiwa baada ya Korea ya Kaskazini kutupilia mbali pendekezo la Kusini, kuhusu mazungumzo juu ya kuanza tena kazi katika eneo hilo la viwanda la Kaesong.
Jana Korea ya Kusini iliipa Kaskazini muda wa masaa 24 kukubali pendekezo hilo, na kuonya kuwa endapo litakataliwa ingechukua hatua muhimu ambazo hata hivyo ilikuwa haikuzitaja. Eneo la viwanda la Kaesong linatoa ajira kwa wafanyakazi wapatao 53 elfu katika kampuni 123 za Korea ya Kusini. Eneo hilo ambalo liko umbali wa kilomita 10 ndani ya Korea ya Kaskazini, ni mfano adimu wa ushirikiano kati ya nchi hizo.
Korea ya Kaskazini iliwaondoa wafanyakazi wake wote tarehe 9 Aprili na kusimamisha shughuli zote, kudhihirisha hasira zake dhidi ya kauli ya Korea ya Kusini kwamba ingepeleka wanajeshi kulinda raia wake katika eneo hilo.

HIZBULLAH NAO WAKANUSHA JUU YA DRONE YAKE

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imekanusha madai kuwa imetuma ndege isiyokuwa na rubani (drone) katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina huko Israel. Jeshi la utawala haramu wa Kizayuni jana lilitangaza kuwa, limetungua ndege isiyo na rubani inayodaiwa kumilikiwa na harakati ya Hizbullah ya Lebanon karibu na bandari ya kaskazini mwa Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Msemaji wa Jeshi la utawala huo alisema kuwa, ndege hiyo ilitambuliwa ikiwa katika anga ya Lebanon katika umbali wa kilometa nane kutoka pwani ya magharibi mwa Haifa na kudondoshwa na jeshi la Israel.
Katika upande mwingine Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon amesema kuwa harakati ya Hizbullah haiingilii masuala ya Syria. Adnan Mansour amesema kwamba, askari wa Hizbullah wapo kwenye vijiji vya mpaka wa Lebanon kwa ajili ya kulinda Walebanoni wa eneo hilo na wala hawashiriki katika operesheni za kijeshi ndani ya Syria.

MUSHARAF AHUSISHWA NA KIFO CHA B.BUTTO

Jenerali Pervez Musharraf rais wa zamani wa Pakistan ametiwa mbaroni kuhusiana na kesi ya mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Benazir Bhutto. Musharraf anatuhumiwa kula njama za mauaji ya Bi. Butto aliyefariki dunia katika shambulizi lililotokea Disemba mwaka 2007. Imeelezwa kuwa, Musharraf anaendelea kubakia nyumbani wake mjini Islamabad anakoshikiliwa kwenye kifungo cha nyumbani kutokana na uamuzi wake wa kuwatimua kazi majaji Novemba mwaka 2007 alipotangaza hali ya hatari nchini humo.
Kukamatwa kwake pamoja na kukosa sifa za kugombea uchaguzi wa Mei 11 vimetoa pigo kubwa kwa kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi wa Pakistan, ambaye alirejea nchini humo mwezi uliopita akiahidi kile alichokiita kuwa ni 'kuiokoa' nchi. Inafaa kushiaria hapa kuwa, hadi sasa hakuna hata mtu mmoja aliyepatikana na hatia au kuhukumiwa kutokana na mauaji ya Bi. Benazir Bhutto, ijapokuwa kesi hiyo imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu sasa.

RUSSIA NA IRAN ZATAKA SYRIA ISIWEKEWE MASHARTI KATIKA MAZUNGUMZO

Iran na Russia zimetoa wito wa kufanyika mazungumzo bila masharti kama njia ya kuhitimisha mgogoro wa Syria uliopelekea maelfu ya watu kuuawa katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa. Wito huo umetolewa katika mazungumzo kati ya Hussein Amir Abdollahian Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na mwenzake wa Russia Mikhail Bogdanov yaliyofanyika hapa mjini Tehran. Wawili hao walijadili pia njia za kusaidia pande za Syria kuanzisha mchakato wa kisiasa utakaoweza kusaidia kuhitimisha mapigano nchini humo.

Katika upande mwingine jeshi la Syria limedhibiti mji muhimu karibu na Damascus baada ya wiki kadhaa za mapigano na waasi wanaofadhiliwa kwa fedha na silaha na nchi za kigeni. Mji huo wa kistratejia wa Otaybah umedhibitiwa na jeshi la Syria baada ya mapigano makali yaliyopelekea waasi wengi kuuawa. Mji huo ulikuwa unatumiwa na waasi kupitishia s

WALIOUWAWA BANGLADESH AJALI YA GHOROFA YAFIKIA 200

Maelfu ya Ndugu na jamaa ya Waathirika wa ajali ya kuanguka kwa jengo nchini Bangladesh waeshuhudia vikosi vya uokoaji vikiwatafuta wapendwa wao katika vifusi vya jengo hilo wakati huu ambapo idadi ya waliopoteza maisha imefikia takriban 200. Ajali hii imezua ukosoaji mkubwa dhidi ya makampuni ya magharibi kuwa yalikuwa yamewekwa mbele kuliko usalama kwa kuweka vyanzo vya bidhaa zao na kutengeneza nchini Bangladesh ingawa nchi hiyo imekuwa na Rekodi ya kupatwa na ajali za namna hiyo. Mamia ya Wafanyakazi walitoka katika viwanda vyao wakiandamana wakati bendera zikipepea nusu mlingoti ikiwa siku ya kitaifa kuomboleza kwa ajili ya wale waliopoteza maisha.
 Sauti za watu kadhaa walionusurika waliofunikwa na vifusi wakiomba msaada zimetoa matumaini lakini Wafanyakazi wa huduma za dharura wametumia siku nzima hii leo kutoa Miili ya Watu. Ajali ya kuanguka kwa jengo lililokuwa na kiwanda cha nguo imeashiria kuwepo kwa tatizo la usalama na Mazingira mabaya ya kufanya kazi vinavyokumba kiwanda hicho kilicho cha pili kwa biashara ya usafirishaji wa Bidhaa kwenda nje. Mwezi Novemba mwaka jana moto mkubwa ulisababisha watu 111 kupoteza maisha katika mji wa Dhaka .

NATO YASEMA IMEFANIKIWA AFGHANISTAN


Majeshi ya jumuia ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO imesema kuwa vita dhidi ya Wanamgambo wa Taliban imeshinda nchini Afghanistani ingawa kumekuwepo na Ripoti za Mashirika mengine kuwa Mashambulizi ya Wanamgambo yameongezeka mwaka huu. Jenerali wa majeshi ya ISAF Joseph Danford amesema kuwa ingawa kumekuwepo na changamoto kadhaa lakini hali ya usalama imeimarika nchini Afghanistani. 
Miongoni mwa Mafanikio yaliyoidhinishwa ni pamoja na kuwawezesha watoto takriban Milioni nane wamekwenda shuleni asilimia 40 wakiwa Wasichana, ikilinganishwa na Watoto Milioni moja ambao wengi wao Wavulana walikwenda shule chini ya utawala wa Taliban wa mwaka 1996-2001. Hivi sasa imeelezwa wanawake wanashikilia zaidi ya asilimia 25 ya viti vya Ubunge halikadhalika Wanawake pia wameanza kujitokeza na kujiunga na Jeshi la Afhanistani.
Kwa Mujibu wa Takwimu za Shirika la utafiti lisilo la Kiserikali Mashambulizi ya Taliban na Wanamgambo wengine yameelezwa kuongezeka tangu mwezi Januari mapaka March mwaka huu ikilinganishwa na kipindi hicho hicho kwa mwaka uliopita. Umoja wa Mataifa umeripoti kuongezeka kwa Mashambulizi kwa na kusababisha madhara kwa Raia kwa asilimia 30 katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Machi mwaka huu.
Kamanda wa majeshi ya ISAF amesema kuwa Operesheni bado inaendelea na kuwa Wanamgambo watapamabana na Majeshi ya Afghanistani na Polisi wa nchi hiyo ambao bado wanaendelea kujiimarisha. Wanajeshi 100,000 wa ISAF watamaliza Operesheni yao mwishoni mwa mwaka 2014 na hivi sasa Vikosi vya kigeni viemanza kuondoka kwa awamu huku Majeshi ya Afghanistan yakitarajiwa kubeba Jukumu la kulinda usalama wa nchi hiyo.

DRONE NYINGINE YA HIZBULLAH YATUNGULIWA ISRAEL

Jeshi la utawala haramu wa Kizayuni limetangaza kutungua ndege isiyo na rubani (dron) inayodaiwa kumilikiwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon karibu na bandari ya kaskazini mwa Haifa huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Shirika la Habari la AP limemnukuu Msemaji wa Jeshi la utawala huo haramu akisema kuwa, ndege hiyo ilitambuliwa ikiwa katika anga ya Lebanon katika umbali wa kilometa nane kutoka pwani ya magharibi mwa Haifa na kudondoshwa na jeshi la Israel. Kwa mujibu wa shirika hilo, ndege iliyokuwa imembeba Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu ambaye alikuwa katika ziara ya kutembelea eneo la kaskazini mwa ardhi hizo za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, ililazimika kutua kwa dharura kufuatia ndege hiyo isiyo na rubani kuingia katika anga ya Israel. Aidha Netanyahu amenukuliwa akisema kuwa, tukio hilo ni zito mno. Hadi sasa meli za utawala huo zinaendelea kutafuta mahali ndege hiyo ilipodondokea. Itakumbukwa kuwa mnamo mwezi Oktoba mwaka jana Israel ilitungua ndege nyengine isiyo na rubani ya harakati hiyo ya Hizbullah suala lililoipelekea Israel kushikwa na wasi wasi mkubwa hadi leo.

WASHINGTON ILIPANGA SHAMBULIO LA BOSTON

Mbunge wa chama cha upinzani cha Republicans nchini Marekani amedai kwamba serikali ya nchi hiyo ndiyo iliyopanga mashambulizi ya mabomu huko Boston wakati wa mashindano ya mbio za masafa marefu maarufu kama Boston Marathon. Stella Tremblay, amesema taarifa ya serikali kuhusu jinsi mashambulizi hayo yalivyotokea haina muwala wala mtiririko na kwa mantiki hiyo inaweza kutiliwa shaka. Amesema kuna ushahidi unaoonyesha kuwa mabomu hayo yalitegwa na serikali ili kufikia malengo yake haramu. Hata hivyo, mbunge huyo wa New Hampshire hakufafanua kuhusu ushahidi huo. Amesema Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kuwaua watu wasio na hatia na kana kwamba haijatosheka, sasa imeamua kumwaga damu za Wamarekani ndani ya nchi yao. Serikali ya Washington haijasema lolote kuhusu tuhuma hizo.

Wednesday, April 24, 2013

MUHADHARA MUHADHARA MUHADHARA


Kutoka page ya ABUU BILAAL SALAFY
Assalaam a'leykum:
Tangazo Tangazo:
Muhadhara Muhadhara:
Wapi:Chuo kikuu cha Dar es salam(MSAUD).
Mhadhiri:Sheykh Abul Fadhli Qaasim ibn Mafuta
Siku:Kuanzia tarehe 26.04.2013(Ijumaa) mpaka 28.04.2013(Jumapili)
Muda:baada ya swala ya Alasiri mpaka i'shay
Mada: Jihaad katika uislam/Jihaad na dhana zake.
*Karibuni wote*

WAFUNGWA WA KIPALESTINA WAZIDI KUPATA TABU ISRAEL

Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel limerefusha kwa miaka miwili zaidi sheria ya kibaguzi dhidi ya Wapalestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala huo. Sheria hiyo iliyopitishwa huko nyuma kwenye bunge ka Israel, inaziruhusu mahakama za Israel kuongeza muda wa kuendelea kushikiliwa jela Wapalestina bila hata kuwepo wenyewe kwenye vikao vya mahakama. Bunge la Israel lilipitisha sheria hiyo miaka miwili iliyopita na kuiwasilisha kwa Baraza la Mawaziri ili irefushwe. Makundi na wanaharakati wa kisiasa wa kutetea haki za binadamu wanaamini kuwa, utawala wa Kizayuni umerefusha muda wa kushikiliwa wafungwa wa Kipalestina ili kuzuia kufichuliwa mateso wanayofanyiwa wakati wanaposhikiliwa. Israel inaamini kuwa, utesaji ni sheria na mateso ni jambo linaloruhusiwa na mahakama za utawala huo. Kwa utaratibu huo kuteshwa wafungwa wa Palestina na Israel ni jambo linalochukua sura mpya kila uchao. Inasemekana kuwa, Israel inatumia kila njia ili kuandaa mazingira ya kuendelea kuwashikilia jela Wapalestina na kuzuia kuachiliwa kwao huru kwa visingizio tofauti. Miongoni mwa njia hizo ni kushikiliwa Wapalestina bila kosa lao kujulikana wala kuhukumiwa. Huo ni ukiukaji wa wazi wa sheria zote za haki za binadamu na za kimataifa, ambapo wafungwa wa Kipalestina wamekuwa wakiendelea kushikiliwa kwa muda mrefu kwenye jela hizo bila kuhukumiwa wala kufahamika tuhuma zinazowakabili. Hii ni katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni unawafanyia kila aina ya jinai mateka wa Wapalestina. Ripoti zinaeleza kuwa, Israel inaendelea kuwapiga sindano za sumu wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala huo, na Wapalestina wametaka kufanywe uchunguzi wa haraka wa kimataifa juu ya suala hilo. Inasemekana kuwa, duru kadhaa za kisheria na za kitiba pia zilitahadhariaha suala la Israel kuwatumia wafungwa wa Kipalestina katika majaribio ya madawa mapya, na kusisitiza kwamba, suala hilo ni kinyume cha misingi ya kimaadili ya taaluma ya tiba. Vyombo vya habari pia huko nyuma vilifuchua ripoti ya siri iliyowasilishwa na  Kamati ya Sayansi ya Bunge la Israel kwa bunge hilo kwamba, kwa mwaka maelfu ya majaribio hatari ya dawa mpya hufanywa kwa kuwatumia mateka wa Palestina, kwa kisingizio cha uchunguzi wa kitiba kwenye jela hizo. Kushtadi hatua hizo za kimabavu za utawala wa Kizayuni dhidi ya wafungwa wa Kipalestina kunadhihirisha kilele cha ukatili huo. Hii ni katika hali ambayo, kukalia kimya jamii ya kimataifa hasa Umoja wa Mataifa jinai  hizo za Israel, kimeufanya utawala huo uendeleze hatua zake hizo dhidi ya Wapalestina hasa mateka wa Kipalestina bila woga wala wasiwasi wowote. La kusikitisha zaidi ni kuwa, licha ya utawala huo kukiuka wazi haki za Wapalestina wakiwemo wafungwa, unaungwa mkono kwa dhati na serikali za nchi za Magharibi suala linaloonyesha kwamba wanakubaliana na kuendelea hatua hizo za ukikaji haki za binadamu na misingi ya kimaadili za Israel.

JOHN KERY ATAKA NATO KUINGIALIA KATI SYRIA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry ameutaka Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) kujiandaa kuingia kijeshi nchini Syria iwapo mambo 'yatakwenda upogo'. Kerry amewaambia Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa NATO mjini Brussels kwamba, muungano wao lazima uwe tayari kujibu shambulio lolote litakalofanywa na jeshi la Syria kwa kutumia silaha za kemikali. Marekani imekuwa ikitoa madai ya uongo kwamba serikali ya Syria imetumia silaha za kemikali dhidi ya raia na makundi ya wapinzani lakini ukweli unaonyesha kwamba yumkini huenda wapinzani wenye kubeba silaha ndio waliotumia silaha hizo kwa msaada wa Marekani. Licha ya tuhuma hizo, Washington imeshindwa kutoa ushahidi kuhusu jambo hilo. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, Marekani sasa inajaribu kutumia muungano wa NATO kufikia malengo yake haramu huko Syria. Hii ni katika hali ambayo, Rais Bashar Asad ameahidi kuendelea kupambana vikali na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na waitifaki wake.

NIGER YAKANUSHA KUPAMBANA NA BOKO HARAM

Waziri wa Ulinzi wa Niger amesema kuwa, jeshi la nchi hiyo halikushiriki kwenye mapigano makali yaliyojiri wiki iliyopita baina ya jeshi la Nigeria na wanamgambo wa kundi la Boko Haram katika eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.
Muhammad Karidio Waziri wa Ulinzi wa Niger amesisitiza kuwa, majeshi ya Nigeria ndio yaliyotekeleza operesheni hiyo ya kijeshi. Waziri wa Ulinzi wa Niger amesema kuwa, kundi la Boko Haram sio tishio la moja kwa moja kwa usalama wa Niger japokuwa Niamey inatoa mashirikiano kwa serikali ya Abuja ya kuliangamiza kundi hilo. Kwenye mapigano yaliyojiri tarehe 19 Aprili, watu wasiopungua 187 waliuawa  katika  eneo la  Baga lililoko Maiduguri, karibu na mpaka wa nchi za Niger na Cameroon.
Afisa mmoja mwandamizi wa jeshi la Niger amesema kuwa, wanamgambo wa Boko Haram tarehe 16 mwezi huu walishambulia doria za majeshi ya Nigeria na Niger katika eneo hilo.

SAUDIA YASIMAMISHA UBOMOAJI WA MISIKITI YA KIZAMANI


Serikali ya Saudi Arabia imelazimika kuacha mpango wa kubomoa mahala alipozaliwa Mtume Mtukufu Muhammad SAW, ili kupanua ujenzi wa Masjidul Haraam baada ya hatua hiyo kukabiliwa na upinzani mkubwa wa wananchi na maulamaa wa nchi hiyo.
A'ref Qadhi Msaidizi wa Mkuu wa Baraza la Mji wa Makka anayehusika na masuala ya ustawi amesema kuwa, maktaba ya Makka haitabomolewa  kwani iko mahala  alipozaliwa Mtume SAW. Hii ni katika hali ambayo, Sheikh Abdul Aziz Aal Sheikh, Mufti wa Kiwahabi nchini Saudi Arabia alitoa fatuwa ya kuruhusu kubomolewa athari za Kiislamu kwa minajili ya kupanuliwa Masjidul Haram.
Naye Sheikh Abdul Wahhab Abu Suleiman ambaye ni miongoni mwa Maulamaa wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu nchini humo amesema kuwa, kubomolewa maktaba hiyo ni sawa na kuondosha athari kubwa zaidi za kihistoria katika dini ya Kiislamu na kwamba suala hilo litaziumiza nyoyo za Waislamu ulimwenguni kote.
Licha ya kufeli zoezi hilo la kubomoa mahala alipozaliwa Mtume SAW, lakini athari nyingine nyingi za kale za Kiislamu zilizoko pambizoni mwa Masjidul Haram zimeshaharibiwa na kubomolewa kwa amri ya utawala kifalme wa Aal Saud.

KENYATTA AANZA KUUNDA SERIKALI YAKE


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya ambapo ametangaza majina ya mawaziri wanne. Wanne hao ni pamoja na Dkt. Fred Okeng'o Matiangi ambaye ni waziri mteule wa Teknolojia na Mawasiliano, Henery Rotich ameteuliwa wizara ya Fedha, James Wanaina Macharia ndiye Waziri mteule wa Afya na Balozi Amina Mohammed ametangazwa Waziri wa mambo ya kigeni.
Ilitarajiwa kwamba Rais Kenyatta angewataja mawaziri wote 18, lakini amesema wengine watatangazwa baadaye na kuomba taifa kuwa na subira. Huku haya yakiarifiwa Bunge la Kenya limeidhinisha kamati maalum ambayo itawachuja mawaziri watakaoteuliwa na Rais. kamati hiyo inaoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi.
Chini ya katiba ya Kenya sharti bunge lipitishe majina ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo Mawaziri, mabalozi na wakuu wa tume za kikatiba.

Tuesday, April 23, 2013

LIBYA YASHEREHEKEA UKOMBOZI


Wakuu wa Libya wametangaza rasmi ukombozi wa nchi katika sherehe iliyofanywa Benghazi, nje ya kambi ambako uasi dhidi ya Kanali Gaddafi ulianza mwezi wa Februari. Kiongozi wa serikali ya mpito, Mustafa Abdel Jalil alisujudu kumshukuru Mungu kwa ushindi wao, huku umati ukishangilia.  Aliwasihi watu wasameheane, wapatane, na kuwa na umoja. Aliwashukuru wote walioshiriki katika mapinduzi - kutoka wapiganaji hadi wafanya biashara na waandishi wa habari waliowaunga mkono.
Alisema Libya itachukua sharia za Kiislamu kama msingi wake.Na alizitakia Syria na Yemen mafanikio katika maandamano yao dhidi ya serikali. Bado hakuna uhakika viongozi wepya wa Libya wataifanya nini maiti ya Kanali Gaddafi.  Kuna taarifa kutoka serikali ya mpito kwamba imeamuliwa kuwa maiti itakabidhiwa kwa jamaa zake. Lakini taarifa nyengine zinaonesha huo siyo uamuzi wa mwisho.

WATUHUMIWA WA UBAKAJI WA MTOTO INDIA WAKAMATWA


Jeshi la polisi nchini India linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za ubakaji wa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano tukio ambalo liliibua hisia kali na kusabababisha maandamano makubwa ya kupinga vitendo vya ubakaji katika mji wa New Delhi. Watuhumiwa hao wawili kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya utekaji na ubakaji wa mtoto huyo. Madaktari katika hospitali ya serikali ya New Delhi wamesema hali ya mtoto huyo kwa sasa inazidi kuimarika na wanaendelea kufanya jitihada kuhakikisha afya yake inakuwa njema.
Aidha waandamanaji wanataka Mkuu wa polisi wa New Delhi aondolewe katika ofisi yake kutokana na jeshi lake kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo kwani limekuwa likipuuza madai mbalimbali yanayowasilishwa kwao. Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh ametoa wito kwa kila mwananchi kushiriki kuwasaidia wanawake na watoto wa kike ambao wamekuwa wakiishi kwa hofu kutokana na vitendo vya ubakaji kuzidi kushika kasi katika nchi hiyo.

Vitendo vya ubakaji kwa wanawake na watoto vimekuwa vikiripotiwa kila uchao katika vyombo vya habari nchini India, miito mbalimbali imezidi kutolewa kwa serikali ya nchi hiyo kuhakikisha wahusika wa makosa hayo wanapewa adhabu kali hasa baada hisia zilizozuka mwishoni mwa mwaka jana baada ya tukio la kubakwa mpaka kufa kwa msichana mwenye umri wa miaka 23 aliyekuwa mwanafunzi wa udaktari. Tayari sheria ya nchi hiyo imefanyiwa marekebisho na kujuisha kipengele cha adhabu ya kifo katika makosa ya ubakaji.

RAIS MUSEVEN ABEBA PESA KWENYE VIROBA


Rais wa Uganda Yoweri Museveni amebuni mbinu mpya ya kuyasaidia Makundi ya vijana nchini mwake kwa kuwakabidhi fedha hizo moja kwa moja kwa lengo la kuepukana na ufisadi ambao umeota mizizi na kuchangia misaada yake kushindwa kuwafikia walengwa. Jumatatu hii Rais Museveni alikabidhi pesa taslimu zipatazo shilingi milioni 25 za Uganda sawa na dola za Marekani laki moja kwa kikundi cha vijana wa Busoga, fedha hizo ziliwasilishwa zikiwa katika gunia suala ambalo limezua hisia mbalimbali kwa wananchi wa Taifa hilo.
Televisheni ta Taifa ya nchi hiyo NTV, ilimuonyesha Rais Museveni akikabidhi fedha hizo, misaada mingine aliyokabidhi kwa vijana wa kikundi hicho cha Busoga Youth Forum ni pamoja na basi dogo, lori na pikipiki 15 ambazo ni ahadi alizozitoa katika kampeni zake za uchaguzi mkuu wa mwaka 2011. Wanaharakati wa kupambana na rushwa na vyama vya upinzani nchini humo wamekosoa hatua ya Rais Museveni kutumia njia hiyo kama mbinu ya kuepukana na suala la ufisadi.
Aidha wakosoaji hao wamesema suala la kupambana na umasikini kwa vijana lilipaswa kuratibiwa na Ofisi ya Rais kwa kufuata taratibu maalumu za serikali na sio Rais kutumia njia hiyo ambayo huenda ikasababisha fedha hizo kutumiwa tofauti na malengo yaliyokusudiwa.

MPANGO WA KIGAIDI TORONTO

Polisi nchini Canada wamewafungulia mashitaka washukiwa wawili kwa kupanga njama ya kuiripua treni ya abiria katika eneo la Toronto. Njama hiyo kubwa ya shambulio la kigaidi imetibuliwa nchini humo kwa usaidizi wa maafisa wa usalama wa Marekani. Maafisa wa usalama wamesema wamekuwa wakiichunguza njama hiyo mjini Toronto na Montreal kwa mwaka mmoja sasa, na wamesema waripuaji hao wanadaiwa kuhusika na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda. Washukiwa hao wawili sio raia wa Canada na polisi nchini humo hawajasema ni raia wa nchi gani. Naibu kamishna wa polisi nchini Canada, James Maliza amesema washukiwa hao hawakuwa karibu na kufanya shambulio hilo. Wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo. 

UBALOZI WA UFARANSA WALIPIUWA NCHINI LIBYA

Ufaransa imelaani shambulio la bomu la kutegwa kwenye gari lililotokea leo kwenye ubalozi wake nchini Libya. Shambulio hilo lililotokea kwenye mji mkuu wa Tripoli, limewajeruhi walinzi wawili. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amesema Ufaransa kwa kushirikiana na viongozi wa Libya watahakikisha wanawabaini haraka wahusika wa shambulio hilo. Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya, Mohammed Abdel Aziz, ameliita shambulio hilo kama kitendo cha kigaidi. Amesema Libya inalaani kitendo hicho dhidi ya taifa lililoisaidia Libya wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 yaliyomuondoa madarakani Muammar Gaddafi. Wapiganaji wamekuwa wakiwalenga wanadiplomasia, ambapo Septemba mwaka uliopita balozi wa Marekani na Wamarekani wengine watatu waliuawa katika shambulio kwenye ubalozi mdogo mjini Benghazi. Wakati huo huo, Fabius leo anaelekea mjini Tripoli, kutokana na shambulio hilo.

RUSSIA KUISAIDIA MISRI MRADI WA NYUKLIA

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Misri amesema kuwa, Russia inakusudia kuisaidia Misri katika kutekeleza miradi ya nishati ya nyuklia nchini humo. Hatim Swaleh ameongeza kuwa, makubaliano ya Russia ya kuisaidia Misri katika nishati ya nyuklia yamefanyika katika safari iliyofanywa wiki iliyopita na Rais Muhammad Morsi wa Misri nchini Russia. Ameongeza kuwa, Russia itaisaidia Misri katika suala la  utafiti kwenye kinu cha nyuklia cha al Dhwaba'a na ustawishwaji wa shughuli za kinu cha kiutafiti cha an Shaasw. Waziri wa Viwanda na Biashara wa Misri amesema kuwa, serikali ya Cairo inataka kupiga hatua mbele kuelekea kwenye mpango wa kujipatia nishati ya nyuklia kwa matumizi ya  amani.

ALI ZIDAN: HATUTOOMBA MSAADA KUTOKA NATO


Waziri Mkuu wa Libya amesema kuwa, nchi yake kamwe haitaomba msaada wa vikosi vya NATO kwa ajili ya kuingilia mgogoro wa ndani nchini humo.
Ali Zidan amekadhibisha vikali uvumi juu ya uwezekano wa kuingilia kijeshi vikosi vya Nato nchini Libya na kusisitiza kuwa, uvumi huo unatolewa kwa shabaha ya kutia doa utendaji wa serikali ya Libya.
Akizungumza na mkuu wa jeshi la polisi na makamanda wa jeshi hilo mjini Tripoli, Zidan amongeza kuwa, wananchi wa Libya wameshuhudia utendaji wa serikali yake na wala hakuna siri yoyote inayofichwa na serikali ya nchi hiyo. Amesisitiza kuwa, serikali ya Libya haijaomba na wala haitaomba msaada wowote kutoka Nato, na hata kama litatolewa, basi bila shaka awali  linapasa kupata baraka za Kongresi ya Taifa la Libya.

TWAHIR AN NUNU: ABBAS AZINDISHA MGANDAMIZO UKANDA WA GHAZA


Msemaji wa Serikali halali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina inayoongozwa na Hamas amesema kuwa, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas ni muungaji mkono mkubwa wa mzingiro kidhulma unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.
Twahir an Nunu Msemaji wa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina amesema kuwa, utendaji wa Mahmoud Abbas unaonyesha wazi kwamba anafanya njama za kudumishwa mzingiro uliowekwa na Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza. An Nunu ameongeza kuwa, 'Abu Mazin' aliitaka serikali ya Marekani imshinikize Raccep Tayep Erdogan Waziri Mkuu wa Uturuki afute safari yake huko Gaza mwezi ujao.
Wakati huohuo Msemaji wa Hamas Sami Abu Zuhri amesema kuwa, takwa la John Kerry Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani kwa Erdogan linaonyesha kuwepo makubaliano kati ya Kerry na Mahmoud Abbas. Katika mazungumzo ya viongozi hao wawili siku kadhaa zilizopita, Kerry alimtaka Erdogan afute safari yake katika eneo la Ukanda wa Gaza.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, utawala wa Israel ulishadidisha mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza mwaka 2007, baada ya Hamas kujipatia ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa bunge la Palestina.

MASANDUKU YA KURA YAIBWA


Kamisheni Huru ya Uchaguzi nchini Ivory Coast imetangaza kuwa, kundi la watu katika eneo la kusini mwa Abidjan hapo jana lilivamia na kupora masanduku ya kura, wakati likiendelea zoezi la kuhesabu kura zilizopigwa katika uchaguzi wa mabaraza ya miji nchini humo.
Msemaji wa Tume Huru  ya Uchaguzi ya Ivory Coast amesema kuwa, karibu watu 200 walivamia eneo la Treichville na kutoweka na makaratasi ya kura, taarifa za uchaguzi na hali kadhailka masanduku ya kupigia kura, huku askari wa usalama waliokuwepo kwenye eneo hilo wakishindwa kuzuia uhalifu huo. Amesema kuwa, hadi sasa haijajulikana ni mrengo gani wa kisiasa uliopanga njama hizo za kupora masanduku ya kura.

ARAB LEAGUE YAKAIDI AGIZO LA BAN KI MOON


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu 'Arab League' amepuuza takwa la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kusimamishwa upelekwaji wa misaada ya kijeshi ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa makundi ya waasi na ya kigaidi nchini Syria.
Nabil al Arabi amesisitiza kuwa, hakuna kitu chochote kitakachoweza kuzuia uungaji mkono wa jumuiya hiyo kwa waasi wanaopambana na serikali ya Syria. Ameongeza, kwa sasa hakuna matumaini ya kutatuliwa mgogoro wa Syria kwa njia za kisiasa.
Hivi karibuni Valerie Amos, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya misaada ya kibinadamu aliliambia Baraza la Usalama kwamba, mauaji yanayofanywa na makundi ya kigaidi dhidi ya wananchi wasio na hatia nchini Syria, kubomolewa majumba na hata vitendo vya  magaidi hao vya kuwatesa  wanawake na watoto vimeshadidisha zaidi mgogoro wa kibinadamu nchini humo.

Monday, April 22, 2013

MTAYARISHAJI WA FILAMU YA KIHOLANZI YA KUMKASHIFU MTUME ASILIMU

Moja ya wanachama wa chama cha Uhuru cha mlengo wa kulia chenye siasa kali nchini uhol...anzi Asilimu. Bwana Arnaud Fandor amesilimu na hivi karibuni katembelea Maka na Madina,baada ya kutoa mchango mkubwa katika kutengeneza filamu ya kumkashifu mtume rehema na amani ziwe juu yake.Gazeti la Okadh online la nchini Saudi arabi limeeleza kuwa liliongozana sambamba na bwana Arnaud Fandor pindi alipoutembelea msikiti wa mtume katika mji wa Madina.
Linasema ya kuwa Arnaud alilia sana pindi alipo litembelea kaburi la mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Bwana Arnaud alisema ya kuwa:Hakika yeye alikuwa ni mwanachama wa chama chenye itikadi kali sana,chenye kuichukia dini ya kiislamu. Anasema pindi alipoona majibu ya waislamu dhidi ya filamu ile,akaamua kuanza kuusoma uislamu na kutaka kujua zaidi siri ya waislamu kuipenda dini yao na mtume wao kiasi hiki.
Bwana Arnaud anasema kuwa shughuli hii ya upekuzi wake juu ya uislamu iemepelekea kugundua ukubwa wa uovu ulio fanywa na chama chake cha zamani,akazidi vutika na uislamu na kutaka kujua zaidi juu ya uislamu kwa kuzidisha kusoma vitabu mbali mbali vya uislamu na kujiweka karibu na waislamu, mpaka akaamua kusilimu.Gazeti hilo pia limemalizia kwa kusema kuwa bwana Arnaud pia kautembelea mlima wa Uhudi. Aliye upande wa kulia katika picha ni bwana Arnaud akiwa radhwa sharifu ndani ya msikiti wa mtume.
 
 
Sources:
 

SERIKALI YAKATAA KUMFUNGULIA KESI MUSHARRAF

 
Serikali ya Pakistan leo imekataa kumfungulia mashtaka ya uhaini, kiongozi wa zamani wa kijeshi wa nchi hiypo, Pervez Musharraf, na imeiambia Mahakama Kuu kwamba hiyo ni zaidi ya mamlaka yake. Hatua hiyo angalau itampa nafuu kidogo, Musharraf ambaye tayari yuko katika kizuizi cha nyumbani kutokana na shtaka moja kati ya matatu yanayomkabili, anayodaiwa kuyafanya akiwa madarakani kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2008. Kesi hizo zinasikilizwa katika mahakama za mwanzo. Musharraf amekuwa akitishiwa kuuawa na kundi la Taliban na amezuiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao. Mahakama Kuu inasikiliza ombi la mawakili wanaotaka Musharraf afunguliwe mashtaka ya uhaini kwa kukiuka katiba. Nchini Pakistan, ni serikali pekee inayoweza kumfungulia mtu kesi ya uhaini, ambayo adhabu yake ni hukumu ya kifo.

WAAFGHANISTAN WASIMAMIE WENYEWE UCHAGUZI WAO

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan ametahadharisha juu ya uingiliaji wowote wa kigeni katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Amesema wananchi wenyewe ndio wanaoapasa kuongoza mchakato wa uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Rais Hamid Karzai aliyasema hayo jana katika mkutano wa baraza la usalama la serikali ya Afghanistan huko Kabul. Katika mkutano huo maafisa wa ngazi ya juu wa Afghanistan pia waliahidi kuwa uchaguzi ujao wa rais utakuwa huru na wa kiadilifu. Itakumbukwa kuwa Rais Hamid Karzai mwaka jana alisema kuwa kuweko wageni katika tume ya kusimamia uchaguzi ya Afghanistan ni dhidi ya kujitawala nchi hiyo. Uchaguzi wa rais wa Afghanistan umepangwa kufanyika Aprili 5 mwaka 2014.

185 WAUAWA KATIKA MAPIGANO NIGERIA

Watu wasiopungua 185 wameuliwa kaskazini mashariki mwa Nigeria katika mapigano kati ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo na wapiganaji wa Boko Haram. Lewa Kole afisa wa serikali za mitaa amemueleza gavana wa jimbo la Borno Kashin Shettima kuwa mapigano yalianza Ijumaa iliyopita huko Baga katika jimbo la Borno na kudumu kwa masaa kadhaa.
Hata hivyo bado haijafahamika ni askari, raia au wanamgambo wangapi wa Boko Haram waliouliwa katika mapigano hayo kwa kuzingatia kuchomwa moto viwiliwili vingi ambavyo havijaweza kutambuliwa, kufuatia moto ulioteketeza karibu mji huo wote. Brigedia Jenerali Austin Edokpaye amesema kuwa raia wengi walitumiwa na wapiganaji wa Boko Haram kama ngao ya binadamu katika mapigano hayo.

MISRI KUMHUKUMU NDUGU WA GHADAFI

Mwendesha mashtaka Mkuu nchini Misri, anakusudia kumpandisha kizimbani mtoto wa ndugu wa dikteta aliyeuawa nchini Libya Kanali Muammar Gaddafi. Ahmed GaddafAl-Dam atapandishwa katika mahakama kuu nchini Misri, kwa tuhuma za kuanzisha mauaji, kupambana na askari wa usalama na kumiliki silaha kinyume cha sheria. Itakumbuwa kuwa, tarehe 19 mwezi Machi mwaka huu, Ahmed GaddafAl-Dam aliwafyatulia risasi Polisi wa Kimataifa Interpol na wa Misri na kumjeruhi mmoja wao, katika oparesheni ya kumtia mbaroni mwana huyo wa ndugu wa Kanali Muammar Gaddafi. Mbali na idara ya mahakama nchini Misri kupinga kumkabidhi Ahmed GaddafAl-Dam kwa serikali ya Libya, imetangaza kumshitaki katika mahakama zake huku ikiwa tayari imekwishatekeleza usaili dhidi yake

POLISI 23 BRAZIL WAFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA

Duru za habari nchini Brazil zinaarifu kuwa, polisi 23 wa nchi hiyo wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha, kwa kosa la kuwaua wafungwa nchini humo. Kwa mujibu wa habari hiyo polisi hao waliohukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka 156, walihusika katika mauaji makubwa zaidi dhidi ya wafungwa 111 katika jela moja ya nchi hiyo mnamo mwaka 1992. Aidha polisi hao 23 ni miongoni mwa polisi 26 ambao walihukumiwa hapo jana na kuachiliwa huru watatu kati yao. Maafisa hao wa polisi ambao wengi wao tayari walikuwa wamestaafu, walihusika katika mauaji ya wafungwa katika jela ya Carandiru iliyopo katika mji wa Sao Paulo mwaka huo uliotajwa. Hata hivyo mawakili wa polisi hao walioitaka mahakama ya Sao Paulo kuwapunguzia adhabu wateja wao, walidai mahakamani kuwa, polisi hao waliwafyatulia risasi wafungwa hao baada ya maisha yao kuwa hatarini.

Sunday, April 21, 2013

LUFTHANSA KUFUTA SAARI ZAKE BAADA YA MGOMO WA WAFANYAZI


Shirikal la ndege la Lufthansa la nchini Ujerumani limesema limefuta nyingi ya safari zake za Ulaya, safari za masafa marefu na hata zile za ndani ya nchi hapo kesho kutokana na mgomo wa wafanyakazi wake wa uwanjani pamoja na wale wa ndani ya ndege.  
Taarifa kutoka kwa shirika hilo imesema imewaweka wafanyakazi 20 kati ya 1,650 kuziba pengo la wafanyakazi waliogoma kushughulikia safari za masafa mafupi hapo kesho Jumatatu na kuonya kuwepo kwa athari kubwa kwa safari za masafa marefu. 
Chama cha wafanyakazi kiliitisha mgomo huo wa kutaka asilimia 5.2 ya nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wa uwanjani 33, 000 wa shirika hilo la Lufthansa baada ya kushindwa kwa duru tatu za mazungumzo ya malipo ya mshahara na viongozi wa shirika hilo.

CHUCK HAGEL ZIARANI ISRAEL


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amewasili nchini Israel hii leo katika ziara yake ya wiki nzima Mashariki ya kati. Katika ziara hiyo Hagel atajadili wasiwasi wa mpango wa nyuklia wa Iran na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Katika ziara yake ya kwanza tangu aliposhika wadhifa huo miezi miwili iliopita waziri huyo pia amepanga kuzungumza na mawaziri wenzake wa eneo hilo juu ya mkataba wa silaha wa euro bilioni 10 utakaozipatia ndege za kijeshi za Marekani pamoja na makombora Israel, Saudi Arabia, na nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.
Amesema mpango huo wa euro bilioni 10 ni ishara tosha kwa Iran kwamba hatua za kijeshi huenda zikachukuliwa kufuatia mpango wake wa nyuklia. 

MAREKANI KUONGEZA MISAA KWA WAASI WA SYRIA


Marekani imesema kuwa itaongeza mara mbili misaada yake kwa upinzani nchini Syria, ikiwa ni pamoja na vifaa vipya vipya vya kijeshi visivyo vya maangamizi, bila kujali wito wa kuuza silaha au kuingilia moja kwa moja. Katika taarifa yake baada ya mazungumzo kati ya marafiki wa Syria wanaounga mkono upinzani wanaokutana huko Istanbul, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alisema msaada wa Marekani kwa upinzani itakuwa ni dola milioni 250 
Hapo jana Muungano wa upinzani nchini Syria uliikosoa urusi na kusema kuwa imeachwa kando na historia kwa kuunga mkono serikali ya rais Bashar al Assad na kwamba inajitenga yenyewe katika uwanda wa kimataifa.

SHUGHUI ZA UOKOAJI CHINA ZAKUMBWA NA CHANGAMOTO


Waokozi bado wanajaribu kuendelea na shughuli ya kutafuta manusura na miili zaidi katika eneo la milimani la Lushan Kusini Magharibi mwa China, baada ya tetemeko kubwa la ardhi lenye kipimo cha ritcher 6.6 kukumba eneo hilo hapo jana.
Huku hayo yakiarifiwa idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko hilo lililosababisha maporomoko ya udongo imepanda na kufikia 203 huku watu wengine 11,800 wakiwa wamejeruhiwa vibaya. Tetemeko hilo liliharibu barabara na kukata mawasilianio ya simu na umeme katika eneo hilo.
Kwa sasa maelfu ya watu wanaendelea kukaa katika mahema wakiwa na hofu kubwa ya kurudi katika eneo hilo.Tetemeko kama hili lilitokea mwaka wa 2008 katika eneo hilo na kusababisha vifo vya takriban watu 70,000.

WAISLAM WAZUIWA KUJENGA MSIKITI UFARANSA

Waislamu wa mji wa Montrouge nchini Ufaransa wamepanga kufanya maandamano makubwa ya kulalamikia hatua ya manispaa ya mji huo ya kupinga kujengwa msikiti mjini humo. Kituo cha habari ya Echo-Montrouge kimewataka Waislamu wa mji wa Montrouge wa kusini mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris, kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano hayo ili kulalamikia hatua ya manispaa ya mji huo ya kuzuia kujengwa kituo pekee cha ibada kwa Waislamu mjini humo. Maandamano hayo yamepangwa kufanyika wiki ijayo yaani Aprili 27, na mkuu wa Jamii ya Waislamu wa Ufaransa, Nabil an Nasri, na mkuu wa jamii ya kupambana na chuki dhidi ya Uislamu, Sami Dabbah, watahutubia waandamanaji na kusisitiza juu ya haki ya Waislamu wa mji huo ya kuwa na msikiti. Jumuiya ya Kudumisha Udugu ya mji wa Montrouge ndiyo iliyoitisha maandamano hayo na imewataka wananchi wote wa Ufaransa kushiriki kwenye maandamano hayo. Ujenzi wa msikiti katika mji wa Montrouge huko Ufaransa ulianza miaka minne iliyopita lakini miezi miwili tu tangu kuanza ujenzi huo, manispaa ya mji huo iliingilia kati na kuzuia kuendelea kujengwa sehemu hiyo ya ibada kwa Waislamu. Waislamu wa Ufaransa walipigania sana haki yao hiyo na mwaka huu wa 2013 wamepewa tena kibali ya kuendelea kujenga msikiti huo lakini hivi sasa pia manispaa ya mji wa Montrouge imeingilia tena kati na kuzuia ujenzi huo kwa madai kuwa Waislamu mjini humo ni wachache hivyo hawana haki ya kuwa na msikiti.

CHINA YAILAUMU MAREKANI KUHUSU HAKI ZA BINADAMU

Serikali ya China imeilaumu vikali Marekani kwa kufumbia macho uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na nchi hiyo katika kila kona ya dunia na badala yake Washington inazituhumu nchi nyingine kukanyaga haki hizo. Taarifa ya Baraza la Mawaziri la China iliyotolewa leo imeongeza kuwa, Marekani imekuwa ikivunja wazi wazi haki za binaadamu kwenye operesheni zake za kijeshi katika kona mbalimbali za dunia na kwa hatua yake ya kuyasaidia kifedha makundi ya waasi ambayo yanavuruga misingi ya kidemokrasia katika nchi mbalimbali duniani. Katika ripoti yake iliyoipa jina "Rekodi ya Haki za Binaadamu Nchini Marekani Mwaka 2012," China imesema pia kuwa, machafuko ya kutumia silaha moto nchini Marekani ni mfano mwingine wa uvunjwaji wa haki za binadamu nchini humo. Imesema, mashambulizi ya kiholela ya kutumia silaha moto yameendelea kuwa tishio kubwa kwa usalama na maisha ya wananchi wa kawaida nchini Marekani. Lawama hizo dhidi ya Marekani zimekuja katika hali ambayo Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa nalo limeilaumu nchi hiyo kutokana na mashambulizi ya ndege zake za kigaidi zisizo na rubani zinazoua watu wa kawaida katika nchi mbali ulimwenguni.

MURSI: USHIRIKIANO NA IRAN SI DHIDI YA NCHI NYINGINE

Rais Muhammad Mursi wa Misri amesema kuwa, siasa za nje za Cairo zinalindwa na maslahi yake ya taifa na kuongeza kuwa uhusiano wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran si kwa madhara ya nchi nyingine yoyote ile. Akizungumza na kanali ya televisheni ya al Jazeera hapo jana, Rais Muhammad Mursi wa Misri amebainisha kuwa Iran ni moja ya nchi za Kiislamu duniani na kwamba wakati Misri inapokuwa na uhusiano na Iran, uhusiano huo hauwi dhidi ya nchi yoyote ile. Tehran ilikata uhusiano wake wa kidiplomasia na Misri baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 nchini Iran kufuatia hatua ya Cairo ya kusaini mkataba wa Camp David na utawala wa Kizayuni wa Israel na kumpa hifadhi Mohammad Reza Pahlavi mfalme aliyepinduliwa na wananchi hapa Iran. Hata hivyo uhusiano kati ya Tehran na Cairo umekuwa ukiboreka kufuatia mapinduzi ya wananchi wa Misri ya mwaka juzi yaliyomng'oa madarakani dikteta wa nchi hiyo Husni Mubarak.

BOKO HARAM YATAKA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SERIKALI

Kundi la Boko Haram ambalo lilihusika na kuwateka nyara raia saba wa Ufaransa limesema kuwa, kuachiwa huru raia hao ni ishara ya juhudi za kundi hilo za kutaka kufanya mazungumzo na serikali ya Nigeria. Muhammad Marwan mwanachama wa kundi la uasi la Boko Haram la nchini Nigeria ametangaza kuwa kitendo cha kuwaachia huru raia saba wa Ufaransa ambao walitekwa nyara tangu miezi iliyopita huko kaskazini mwa Cameroon karibu na mpaka na Nigeria, kunaonyesha kuwa kundi hilo lina nia ya kufanya mazungumzo na serikali. Marwan amesisitiza pia kwamba, kuachiwa huru raia hao wa Ufaransa kumekuja baada ya mashauriano kati ya wakuu wa Boko Haram kama juhudi za kuanzisha mazungumzo na kurejesha utulivu huko Nigeria. Siku kadhaa zilizopita Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria alisema kuwa kumeundwa kamati ya watu 26 waliopewa jukumu la kuchunguza uwezekano wa kuwasamehe wanachama wa kundi la Boko Haram kwa shabaha ya kurejesha amani nchini humo.

TETESI KUHUSU UCHAGUZI WA RAIS IRAN

WAGOMBEA KITI CHA URAIS IRAN

Huku uchaguzi wa rais ukikaribia nchini Iran, joto la kisiasa linaendelea kupanda baada ya kuwepo tetesi kuhusu uwezekano wa kugombea tena marais wa zamani Akbar Hashemi Rafsanjani na Seyyed Mohammad Khatami.
Kwa mujibu wa Press TV, Mohammad Reza Aref ambaye alikuwa makamu wa kwanza wa rais Khatami amesema atajiondoa iwapo rais huyo wa zamani atagombea urais katika uchaguzi wa mwezi Juni. Hata hivyo mgombea Mohsen Rezaei amesema hatajiondoa hata kama marais wa zamani Rafsanjani na Khatami watagombea. Kwa mujibu wa sheria ya Iran, rais wa zamani anaweza kugombea urais baada ya kupita miaka mitano ya kumalizika muhula wake. Wakati huo huo mbunge mwandamizi Alireza Zakani naye amejitosa katika kinyang'anyiro cha urais nchini. Zakani ambaye ni katibu mkuu wa Jumuiya ya Wafuasi wa Mapinduzi ya Kiislamu alitangaza uamuzi wake Jumamosi usiku. Aidha waziri wa zamani wa afya Kamran Bagheri Lankarani ametangaza kugombea urais kwa tikiti ya Mrengo wa Waibua Hamasa ya Mapinduzi ya Kiislamu. Wengine waliotangaza nia ya kuwania urais wa Iran ni pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Mostafa Pour-Mohammadi, mwanachama mwandamizi wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo, Hassan Rohani na waziri wa zamani wa mambo ya nje Manoucher Mottaki. Rais Mahmoud Ahmadinejad anamaliza muhula wake wa pili na hivyo kikatiba hawezi kugombea. Uchaguzi wa rais Iran utafanyika Juni 14 na wagombea watajiandikisha kati ya Mei 7 na 11.

NAIBU MKUU WA HIZBULLAH ASEMA WAKO TAYARI KWA NJAMA ZOZOTE ZA ISRAEL NA MAREKANI


Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kwamba, harakati hiyo imejiandaa kikamilifu kwa ajili ya kukabiliana na njama za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mashariki ya Kati. Sheikh Nabil Qaouq amesema kuwa, kuna haja ya kuendelezwa muqawama dhidi ya maadui na kwamba, muqawama ni dharura ya kitaifa na stratejia kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya utawala haramu wa Israel ambao unataka kuutumia vibaya mgogoro wa sasa wa Syria.
Sheikh Nabil Qaouq amesisitiza kwamba, katika hali ya hivi sasa Hizbullah iko katika hali nzuri kabisa ya maandalizi, jambo ambalo hata Ehud Barak, waziri wa zamani wa vita wa Israel amelikiri bayana. Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, kama ambavyo muqawama ulipata ushindi mbele ya utawala wa Kizayuni wa Israel utazishinda pia njama za Marekani kwa kuitisha uchaguzi na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa nchini Lebanon.

Saturday, April 20, 2013

MALI KUFANYA UCHAGUZI JULAI

Rais wa mpito wa Mali, Dioncounda Traore amewahakikishia washirika wa kimataifa kwamba nchi yake iko tayari kufanya uchaguzi wa kidemokrasia ifikapo mwezi Julai mwaka huu, kama alivyoahidi. Matamshi hayo ameyatoa kwenye mji mkuu wa Bamako, mwanzoni mwa mkutano wa wajumbe wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS. Rais Traore amesema kutokana na msaada wa marafiki wa Mali, uchaguzi wa nchi hiyo utafanyika kwa muda uliopangwa. Amesema nchi hiyo inayopambana na waasi wenye itikadi kali za Kiislamu iko salama, ingawa bado juhudi zaidi zinahitajika kuimarisha usalama. Katika tamko lililotolewa mwishoni mwa mkutano huo, wajumbe wamefurahishwa na hatua ya kufanyika kwa uchaguzi wa urais mnamo Julai 7 na wa wabunge utakaofanyika Julai 21.

MSHUKIWA NAMBA 2 WA BOSTON ATIWA NGUVUNI

Polisi nchini Marekani inamshikilia kijana mmoja anayedhaniwa kuhusika na mashambulizi yaliyojitokeza katika mbio za marathon za mjini Boston mapema juma hili. Kijana huyo Dzhokhar Tsarnaev mwenye umri wa miaka 19 alikutwa mafichoni alipokuwa amejihifadhi baada ya mshukiwa mwenzie kuuawa katika majibizano makali ya risasi na polisi umbali wa kilomita kumi kutoka Boston.

Ripoti mbalimbali za vyombo vya habari toka nchini humo zinasema mshukiwa huyo alikutwa amejificha kwenye akiwa na majeraha aliyoyapata katika makabiliano baina yao na polisi ambayo yalipelekea kifo cha kaka yake Tamerlan ambaye ni mshukiwa wa pili katika tukio hilo.

Ndugu hao wawili wanadhaniwa ndio waliotega mabomu mawili karibu na mstari wa mwisho wa mbio za marathon za Boston siku ya jumatatu, tukio ambalo lilisababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa.

Kamishna wa polisi wa Boston Ed Davis amewaambia waandishi wa habari hali ya mshukiwa huyo ni mbaya sana kutokana na majeraha aliyonayo na anapatiwa matibabu katika hospitali moja mjini humo.

Akizungumza baada ya kukamatwa kwa mshukiwa wa pili, Rais wa Marekani Barack Obama ameapa kuhakikisha wanampata mtu aliyewatumia vijana hao wawili kama chambo ya kutekeleza mashambulizi hayo.